School ConnectivityTanzania · East Africa
HomeAboutTeamNewsPublicationsGalleryContact Us
© School Connectivity
Back to all news

UDOM yaonesha nguvu ya tafiti na ubunifu wa kidijitali kuelekea Tanzania 2050

26 June 2026DodomaSchool Connectivity Team
UDOM yaonesha nguvu ya tafiti na ubunifu wa kidijitali kuelekea Tanzania 2050

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kupitia Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu (CIVE), kimezindua rasmi Wiki ya Utafiti na Ubunifu, ikianza kwa maonesho ya tafiti na bunifu za kidijitali zinazolenga kutoa suluhisho bunifu kwa changamoto za jamii na kuchochea maendeleo endelevu ya Taifa.



Maonesho hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “Ubunifu wa Kidijitali kwa Tanzania 2050: Kuchochea Mabadiliko na Kuwezesha Maisha ya Watu,” yakilenga kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kidijitali kama chachu ya maendeleo kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania 2050.

Akifungua rasmi maonesho hayo yaliyofanyika katika viunga vya Ndaki ya CIVE “Auditorium” Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohamed Mashaka, alisema ubunifu wa kidijitali ni msingi muhimu wa maendeleo ya Tanzania ya baadaye.

Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono tafiti na bunifu zinazobuniwa na vijana pamoja na wataalamu wa Kitanzania ili kuzalisha suluhisho endelevu kwa changamoto za kijamii, kukuza uchumi wa kidijitali na kuongeza ushindani wa taifa katika nyanja za teknolojia na ubunifu.

Soma zaidi Hapa

Last updated: 26 June 2026
Share this story:

You might also like

Continue reading more stories from our community

UDOM NA NMB WAHAMASISHA VIJANA KUTUMIA TECHNOLOGIA NA UBUNIFU KUJENGA MUSTAKABALI WAO
25 Jun 2026

UDOM NA NMB WAHAMASISHA VIJANA KUTUMIA TECHNOLOGIA NA UBUNIFU KUJENGA MUSTAKABALI WAO

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kupitia Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu kwa kushirikiana na Benki ya NMB, kimeandaa mhadhara wa wazi wa kitaaluma uliolenga kuwawezesha w...

UDOM, UNICEF WALETA MAPINDUZI YA KIDIJITALI KONDOA
25 Jun 2026

UDOM, UNICEF WALETA MAPINDUZI YA KIDIJITALI KONDOA

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Bi. Rose Joseph, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Amani Abeid Karume kuhusu fursa za kujifunza kidijitali, wakati wakikag...

UDOM and UNICEF Tanzania Joined to Support School Connectivity Programme
25 Jun 2026

UDOM and UNICEF Tanzania Joined to Support School Connectivity Programme

Towards Sustainable Schools and Communities InternetConnectivity Programme using TV Digital White Space On 14th March 2022, The University of Dodoma (UDOM) and UNICEF Tanzania has...