Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Bi. Rose Joseph, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Amani Abeid Karume kuhusu fursa za kujifunza kidijitali, wakati wakikagua huduma ya mtandao imavyofanya kazi shuleni hapo na kusaidia wanafunzi kujifunza.

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa kushirikiana na UNICEF Tanzania, kimeanza kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya kidijitali katika Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, kupitia mradi wa kusambaza huduma ya intaneti kwa shule na jamii.
Katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo iliyofanyika leo Alhamisi, tarehe 19 Machi 2026, ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Bi. Rose Mdami, imeelezwa kuwa hatua kubwa tayari imefikiwa.
Msimamizi wa mradi huo, Dkt. Jabhera Matogoro, amesema vituo 10 tayari vimeunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi ya 20Mbps, ikijumuisha shule tano za sekondari na Msingi, na vituo vitano vya jamii, hatua inayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika upatikanaji wa taarifa, ujinzaji na ufundishaji.
Ameeleza kuwa mradi huo unalenga kuwezesha walimu, wanafunzi na wananchi kwa ujumla kupata maarifa kwa urahisi kupitia mtandao, sambamba na kuchochea fursa za ajira, ubunifu wa kibiashara na maendeleo ya kijamii katika wilaya hiyo.
Soma zaidi Hapa



