School ConnectivityTanzania · East Africa
HomeAboutTeamNewsPublicationsGalleryContact Us
© School Connectivity
Back to all news

UDOM NA NMB WAHAMASISHA VIJANA KUTUMIA TECHNOLOGIA NA UBUNIFU KUJENGA MUSTAKABALI WAO

25 June 2026DodomaSchool Connectivity Team
UDOM NA NMB WAHAMASISHA VIJANA KUTUMIA TECHNOLOGIA NA UBUNIFU KUJENGA MUSTAKABALI WAO

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kupitia Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu kwa kushirikiana na Benki ya NMB, kimeandaa mhadhara wa wazi wa kitaaluma uliolenga kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa na ujuzi unaohitajika katika uchumi wa kidijitali na soko la ajira la sasa.

Mhadhara huo uliofanyika Jumatano ya tarehe 24 Juni 2026 uliendeshwa chini ya kaulimbiu isemayo “Ubunifu wa Kidijitali, Maendeleo ya Vipaji na Uongozi Unaotazama Mustakabali kwa Ajili ya Dira ya Tanzania 2050.”

Akifungua mhadhara huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, aliipongeza Benki ya NMB kwa ushirikiano wake na UDOM katika kukuza elimu, ubunifu na maendeleo ya vijana, huku akisisitiza umuhimu wa wanafunzi kutumia teknolojia kama nyenzo ya kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi huku wakijiandaa kushiriki kikamilifu katika mageuzi ya kidijitali yanayoendelea duniani.

Prof. Kusiluka alisema mhadhara huo ni sehemu ya maandalizi ya Wiki ya Ubunifu ya UDOM 2026 (CIVE Innovation Week 2026) na unalenga kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri kwa ubunifu, kuendeleza vipaji na kutumia teknolojia kuleta suluhisho zenye tija kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake, Meneja Mahusiano kati ya Benki na Taasisi wa Benki ya NMB Plc, Kanda ya Dodoma, Bw. Festo Mwakasengo, alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi za elimu ya juu nchini katika kuwawezesha vijana kujenga ujuzi, ubunifu na uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya uchumi wa kidijitali.

Soma Zaidi Hapa

Last updated: 1 July 2026
Share this story:

You might also like

Continue reading more stories from our community

UDOM yaonesha nguvu ya tafiti na ubunifu wa kidijitali kuelekea Tanzania 2050
26 Jun 2026

UDOM yaonesha nguvu ya tafiti na ubunifu wa kidijitali kuelekea Tanzania 2050

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kupitia Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu (CIVE), kimezindua rasmi Wiki ya Utafiti na Ubunifu, ikianza kwa maonesho ya tafiti na bunifu za...

UDOM, UNICEF WALETA MAPINDUZI YA KIDIJITALI KONDOA
25 Jun 2026

UDOM, UNICEF WALETA MAPINDUZI YA KIDIJITALI KONDOA

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Bi. Rose Joseph, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Amani Abeid Karume kuhusu fursa za kujifunza kidijitali, wakati wakikag...

UDOM and UNICEF Tanzania Joined to Support School Connectivity Programme
25 Jun 2026

UDOM and UNICEF Tanzania Joined to Support School Connectivity Programme

Towards Sustainable Schools and Communities InternetConnectivity Programme using TV Digital White Space On 14th March 2022, The University of Dodoma (UDOM) and UNICEF Tanzania has...